Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Ujumbe wa wanazuoni wa Kiislamu kutoka Russia umefika nchini Iran kwa ajili ya kutoa heshima na kuaga mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Umma wa Kiislamu, Imam Sayyid Ali Husayni Khamenei (Qudsallahu Nafsahu az-Zakiyyah).
Ujumbe huo ulitoa salamu za rambirambi na kusisitiza nafasi muhimu ya kiongozi huyo katika kuimarisha umoja wa Waislamu, kutetea waliodhulumiwa na kuunga mkono harakati za Muqawama duniani.
Hafla hiyo imeendelea kushuhudia ushiriki wa viongozi wa dini, wanazuoni na wajumbe mbalimbali kutoka mataifa tofauti wanaofika kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo mashuhuri wa Umma wa Kiislamu.
Your Comment